Through the mind’s eye
Behold distant skies!
Discern you, a cataclysm
Staring at us
Like bubonic plague provoked
Arrogant chemicals
Masticate the ozone
Like armies of ants
In an invasion of a roof
Of rafters
Were it we
Who, with know-how
Assembled the ozone in sky
And hang it in the skies
Like a master builder
Thatching a roof
This cloud of anxiety
Wouldn’t be this heavy
In the weighing scales of the heart
For the expertise to invent
Is knowledge to rectify
But Ozone, oh Ozone,
We found you in place!
Without hurting my minds
With painful payments
You accepted sheltering us
From dangerous stomach gases
Born of the sun’s abdomen
Thank you, shield of life
You, sheltering us from fatality
Like invincible bunker
Concealing the citizens
From missiles
Of terrible brigades
Oh, we humanfolk!
With foolhardy technology
We enfeeble your health
While death, our enemy
Gazes at us
Ready to attack
Kwa macho ya akili
Tazama anga za mbali!
Unaona jinsi janga
Linavyotukodolea macho
Kama tauni iliyochokozwa?
Kemikali jeuri
Zinatafuna Ozoni
Kama majeshi ya mchwa
Yaliyovamia paa
La kombamoyo
Ingelikuwa ni sisi
Ambao kwa ujuzi wetu
Tuliunda Ozoni
Tukaitundika angani
Kama mjenzi mahiri
Akiezeka paa la nyumba
Hili wingu la wasiwasi
Lisingelifikia huu uzani
Katika ratili ya moyo
Kwani kujua kuunda
Ni kujua kurekebisha
Lakini Ozoni, ewe Ozoni
Tilikukuta ulipo!
Bila kutuumiza akili
Kwa uchungu wa malipo
Ulikubali kutukinga
Kutokana na uzushi hatari
Kutoka tumbo la jua
Asante, ngao ya uhai
Unayetulinda kutokana na mauti
Kama handaki imara
Ikisitiri wakazi wa mji
Kutokana na makombora
Ya vikosi vikali
Ole wetu, sisi binadamu!
Kwa teknolojia jeuri
Tunakulegeza afya
Huku adui mauti
Akituangalia
Tayari kutushambulia
Poems by Prof. Kithaka Wa Mberia