POETIC HEART – 5

by. Prof. Kithaka Wa Mberia

Since the knock on the door by the message of invitation

Until the day of the flight by wings of metal

Digital letters spoke in a crystal-clear language

Informing me with words passed through a sieve

What I had to know for the trip to be as smooth as satin

The trip to Dubai was without huddles to handle

At the airport the guest witnessed courtesy

The reception was organized with sparkling precision

The alighted passenger wasn’t pursued by the heat of solitude

Loneliness had no chance of laughing at the poet

In the hotel, preparations hadn’t a gap to plug in

There weren’t questions smelling of humiliation

Service lenders received me with joyful hands

The bedroom welcomed me with smiles

Embraced me evaporating the journey’s fatigue

In a session to congregate the visitors and the hosts

Did meet the eyes, hands, hearts and smiles

The auditorium reverberated with dignity and togetherness

With an accord without the raising of a compelling voice

We constructed a map to guide the enthusiasts along the way

When the sun opened the curtain of sky of the day of the recital

In the Nadwat Al-Thaqatah wa Al-Uloom Buildings

Welcomed we were with snacks laced with smiles

Sat we in breezes of discipline and dignity

Excitedly mingling with a graceful audience

In an auditorium adroitly designed and decorated

Facilitators elegantly adorned and charismatic

Bid welcome to the crowd with pulsating respect

Introducing the poets with shiny words

The session become a glorious party for eyes and ears

In turns, audaciously, the poets mounted the podium

Their pleasant tongues entertained with elegant speech

The rhythm of compositions vibrating with graceful beats

In the hearts of the audience happiness blossomed like flowers

Excitement ruled the hall and into the skies emotions rose

When the second day opened the door and welcomed the crowds

Besides the experts wearing gowns of precious experience

Faces of budding artists shone in the auditorium

Their uniform adorning the surrounding s like flowers in garden

With glorious elegance reciting deep pieces

The audience was delighted by bards and the audacious debutants

None raised the query, “What really went astray”?

We abundantly clapped to congratulate and urge on

None on the podium was heart-broken or in regret

The artists and the audience united in merriment

What tranquility travelling by the vessel of Poetic Heart

What happiness being in a rainbow of creativity

Beholding the elderly and the youth floating up in the clouds

Waving metaphors in languages of graceful cultures

Advocating togetherness of the dwellers of nations?

Congrats whoever dreamed of lighting this precious firebrand

That has given birth to this light for congregating bold hearts

A worthy move against the darkness of intolerance in the world

So as, with cultures embraced in genuine feelings

There emerge a new life dazzling with peace Moyo wa Ushairi - 5

Tangu kubishiwa hodi na ujumbe wa mwaliko 

Hadi siku ya kuruka kwa mabawa ya madini

Nyaraka mtandaoni ziliongea kwa lugha fasihi

Zikiarifu kwa maneno yaliyopitishwa kichungini

Niliyopaswa kujua ziara yangu iwe laini ja hariri

Ziara ya Dubai haikuwa na kihunzi za kutatua

Katika uwanja wa ndege mgeni aliona taadhima 

Mapokezi yalipangwa kwa utaratibu uliong’aa

Kushuka abiria hakukufuatwa na joto la ukiwa

Upweke haukupata nafasi ya kuchekelea mshairi

Hotelini maandalizi hayakuwa na pengo la kuziba

Hakukuwa na maswali yenye harufu ya udhalilishaji

Wahudumu walinipokea kwa mikono mikunjufu

Chumba cha kulala kikanikaribisha kwa tabasamu

Kikanipiga pambaja na kuvukiza machovu ya safari

Kwenye kikao cha kujumuisha wageni na wenyeji

Yalikutana macho, mikono, nyoyo na tabasamu

Ukumbi ukarindima kwa heshima na utangamano 

Kwa maafikiano bila kupanda sauti ya kushurutisha

Tukaunda ramani ya kuongoza njia wakereketwa

Jua lilipofungua pazia la anga la siku ya utongoaji

Kwenye jengo la Nadwat Al-Thaqafah wa Al-Uloom

Tulilakiwa kwa vitafunio vilivyopakwa tabasamu

Tukaketi kwenye pepezi za nidhamu na heshima

Kwa ukunjufu tukitangamana na hadhira pendezi

Ukumbini uliosanifiwa na kupambwa kwa umahiri 

Waratibu wenye ulimbwende na haiba ya kilele

Walikaribisha umati kwa taadhima iliyorindima

Na kutambulisha washairi kwa maneno maangavu

Kikao kikawa karamu murwa kwa macho na masikio

Kwa zamu washairi walipanda jukwani wakivaa ujabari

Lugha zao pendezi zikatumbuiza kwa matamshi jamala 

Mdundo wa tungo ukirindima kwa mapigo matamu

Katika nyoyo za hadhira furaha ikachanua kama mawaridi

Msisimko ukatamalaki ukumbi na kukweza hisia angani

Siku ya pili ilipofungwa mlango na kukaribisha umati 

Mbali na gwiji waliovalia magwada  ya tajriba adimu 

Nyuso za wasanii chipukizi zilinawiri katika ukumbi 

Sare zao kipamba mandhari kama maua katika bustani

Wakatongoa mashairi yenye uketo kwa umbuji bulibuli

Hadhira ilichangamkia gwiji na wanachipukizi jasiri

Kusiwe wa kuulizwa, “Je, mambo yamekwandaje?”

Tukapiga makofi tumbitumbi kupongeza na kuhimiza

Jukwaani kusiwepo aliyevunjika moyo au kujutia hali

Wasanii na hadhira wakachanganyika kwenye bashasha

Utuvu ulioje kuabiria chombo cha Moyo wa Ushairi

Furaha ilioje kuwa katika upinde wa mvua wa utunzi

Kuona wazee kwa vijana wakielea juu mawinguni

Wakipeperusha jazanda kwa lugha za tamaduni aali

Wakipigia debe kutangamana kwa wakazi wa mataifa?

Heko kwa aliyewazia kuwasha huu mwenge adimu 

Ukazaa huu mwangaza wa kujumuisha nyoyo jasiri

Hatua azizi dhidi ya giza la kutovumiliana duniani

Ili kwa tamaduni zilizokumbatiana kwa hisia halisi

Yazuke maisha mapya yanayometameta kwa amani