Game of Cards

by. Prof. Kithaka Wa Mberia

We sat, facing each other

 In life’s parlour

Two factions, we were

One, ours

The other, of ogres

Playing a game of cards

In our team

We discerned, all along

That game of cards

Wasn’t going to be easy

Because ogres

 Are full of crafty schemes

 But we didn’t dull our dream

We heartened our resolve

When the game started

We cast a card

They cast a card

We cast a card

They cast a card

Cunningly, they won the round

In the following round

 We cast a card

They cast a card

We cast a card

They cast a card

We drew a card

Our ace trophy card

Trusting it to succeed

In tilting the scales

In our favour

When this became evident

The High Councilof ogres

Changed the rules

The ace card we intended

Was outlawed,

From the game

In the next round

We cast a card

They cast a card

We cast a card

They cast a card

We casting a card

They casting a card

This game of cards

Is exhausting our muscles

Like climbing a mountain

But we won’t dull our dream

Of victory in this parlourMCHEZO WA KARATA

Tuliketi, tukiangaliana

Kwenye ukumbi wa maisha

Tulikuwa vikundi viwili  

Kimoja chetu  

Kingine cha mazimwi  

Tukicheza karata  

Katika kundi letu  

Tulielewa tangu mwanzo  

Kwamba ule mchezo  

Haungekuwa mwepesi  

Kwani mazimwi  

Wana hila chungu  

Bali hatukulegeza ndoto  

Tulijikaza moyo  


Ulipoanza mchezo  

Tulitupa karata  

Wakatupa karata  

Tukatupa karata  

Wakatupa karata  

Kwa ujunja wakashinda hiyo duru  


Kwenye duru iliyofuata  

Tulitupa karata  

Wakatupa karata  

Tukatupa karata  

Wakatupa karata  

Tukashika karata  

Yenye uzito ambao  

Tuliamini ungefaulu  

Kuinamisha ratili  

Upande wetu  

Hili lilipobainika  

Kamati Kuu ya Mazimwi  

Ilibadilisha masharti  

Ile karata tuliyoazimia  

Ikawa marufuku  

Kwenye mchezo  

Kwenye duru iliyofuata  

Tulitupa karata   

Wakatupa karata  

Tukatupa karata   

Wakatupa karata. . .  

Tukatupa karata   

Wakatupa karata. . .  

Huu mchezo wa karata  

Unatuumiza misuli  

Kama upandaji mlima  

Bali hatukulegeza ndoto 

Ya ushindi ukumbini